Pages

Subscribe:

Saturday, October 13, 2012

Namna Ya Kubadilisha Operating System~ Windows Xp


Kwanza inatakiwa uilazimishe mashine yako iweze kuwaka(boot) kutokea kwenye cd na sio hard disk kama inavyowaka katika hali ya kawaida.
Kuna njia mbili za kuseti muwako huo, unaweza kuiseti(set) na kuhifadhi aina hiyo ya muako(boot sequence) na kisha utaizima na kuiwasha mashine yako, moja kwa moja itaanza kuwaka tokea kwenye cd, ili uweze kuiset namna hii, unatakiwa ubonyeze bonyeze kifungo F2 au F1 wakati mashine inaanza kuwaka tu( kioo wakati huo kitakuwa cha rangi nyeusi, kabla haijafika kwenye Os(windows) wakati huo tunasema mashine inboot) baadhi ya mashine hua zinatoa maelekezo kama yafuatayo “Press F2 for setup, na chini wanaandika Press F10 for boot order” jumbe hizi ni kama msaada kwako ili uweze kujua ni vifungo gani vitaweza kukupeleka sehemu ambayo unaitaka. Nimeandika F1 au F2 ndio vitaweza kukupeleka kwenye eneo ambalo utaweza kuset aina ya muako nikiwa na maana, mashine hutengenezwa na kampuni tofauti(manufacturer) hivyo vifungo vya kukupeleka eneo ambalo utaweza kuset aina ya muako huachiana kwenye baadhi ya mashini lakini mara nyingi F2 ndio hutumika katika kompyuta nyingi.
Ikifunguka kurasa(window/page) hiyo ambayo utaweza kufanya marekebisho tafuta eneo ambalo utaweza kuona boot sequence/boot order ili uweze kubadili. Namna ya kuifikia page husika pia huachiana lakini kama utakuwa makini window hiyo itakayofunguka itakupa maelezo ya namna ya kufika page moja mpaka nyingine, kwamfano Dell D610 wakati ikiwa inaanza kuwaka kama utafanikiwa kubofya F2 itakupeleka kwenye page ya mwanzo ambayo itakuonesha tarehe na sifa(specification ) za mashine, na ili uweze kufikia page nyingine utatakiwa ubonyeze Alt (hold) na P (press), akibonyeza Alt na P itakupeleka page ya pili yenye kichwa cha kurasa “Boot Order” na page hii ndiyo tunayoitaka , utaona orodha(list) ya vifaa tofauti ambavyo mashine itaweza kuweka kama OS(Windows/bootble device) itawekwa humo, kwa mfano mashine hiyo ya dell inaorodha hii.
Diskette Drive
Internal HDD (hard disk)
Usb Storage Device
CD/DVD/CD-RW Drive
Modular Bay HDD
Cardbus NIC
D/Dock Slot NIC
Onboard NIC
Namna orodha ilivyo ndivyo ilivyo Boot Order, kwaamana mashine yako ikiwaka itaanza kuangalia kwenye diskette kama kuna Os (windows/bootable device) kama hakuna itakwenda kuangalia kwenye hard disk kama windows nzima(bootable device) itakutwa humo mashine itawaka kutokea kwenye hard disk, haitokwenda tena kuangalia kama kuna windows kwenye USB(flash) au Cd Rom n.k, Orodha hiyo unaweza kuibadilisha mtililiko wake ili uilazimishe mashine iwake(boot) kutokea uitakayo. Sasa kama unataka kubadilisha Operating System(windows) yake kwa kutumia cd unatakiwa Upandishe CD/DVD/CD-RW Drive iwe ya kwanza katika Orodha hiyo, yani ionekanae kama ifuatavyo.
CD/DVD/CD-RW Drive
Diskette Drive
Internal HDD (hard disk)
Usb Storage Device
Modular Bay HDD
Cardbus NIC
D/Dock Slot NIC
Onboard NIC
Au

CD/DVD/CD-RW Drive
Internal HDD (hard disk)
Diskette Drive
Usb Storage Device
Modular Bay HDD
Cardbus NIC
D/Dock Slot NIC
Onboard NIC

Au vyovyote vile lakini CD Rom iwe ya kwanza kama unataka kubadili OS(windows) kupitia CD , kwasbb windows Os inaweza kubadilishika kwa njia nyingi kwamfano USB(flash/Memory Card), kwa njia ya Network N.k lakini njia ya CD ndio Maarufu zaidi.
Sasa namna ya kubadili mtiririko huu unategemea aina ya mashine lakini kwa Dell niliyoitaja hapo juu utabonyeza kifungo chenye herufi “U” kupandisha juu kitu ulichokichagua na herufi “d” utaitumia kushusha chini ya orodha , maelezo ya vifungo na matumizi yake yenyewe mashine itakuoneyesha.
Maelezo ya mfano kwenye ukurasa(windows) huo wa “boot order”
“Press “u” or “d” to move a device up or down in the list.”
“Press the SPACEBAR to enable or disable a device. Enable Devices”
Baada ya kubadili na kuifanya Cd/DVD Rom ndio ya mwanzo katika “boot order’ , utabonyeza kifungo cha escape lakini kwenye kibodi yako kimeandikwa Esc , ukibonyeza kifungo hiko itatokea page yenye ujumbe huu.
“What do you want to do?
Save changes and exit
Discard changes and exit
Return to setup
Note : Most Changes require a system reboot before taking effect “
Utachagua “Save Changes and exit” alafu utabonyeza enter
Hapo utakuwa tayari umebadilisha boot order, hivyo kinachokupasa ni kuweka CD yenye OS(windows) na cd/dvd kama ni bootable itasoma maelezo haya “Press any key to boot from cd” ukiwa na maana bonyeza kifungo chochote ili uweze kuiwasha mashine yako(boot) kwa kutumia cd/dvd, hivyo kwasbb unataka kubadili OS(windows) kutokea kwenye cd/dvd itakupasa obonyeze kifungo chochote.

Kuna njia ya mkato(njia ya pili) itawakayo weza kukupeleka kwenye Boot order hasa kwenye mashine za Michael Dell maarufu kama Dell, wakati mashine inaanza kuwaka utatakiwa ubonyeze F12 , kama umeipatia itasimama katika hali hiyo hiyo ya weusi na kukufungulia page yenye boot order na itatoa orodha kama ifuatayo.

Internal HDD (hard disk)
CD/DVD/CD-RW Drive
Cardbus NIC
Onboard NIC
Diagnostics
Baada ya kuja orodha hiyo, utaweka cd yako ya Os (windows) baadae utatumia vifungo vya kushusha chini na juu(Arrow) utachagua CD/DVD/CD-RW Drive na kubonyeza (Press) Enter , mashine itaanza tena kuwaka na kukuletea ujumbe huu “Press Any key To Boot From Cd” utabonyeza kitufe chochote na mashine itaanza kuboot(kuwaka) kutoka kwenye cd/dvd iliyopo kwenye cd au dvd rom.


Tunaanza na kuelekezana namna ya kubadilisha windows Xp kwasababu ndio inayotumika zaidi, inatumika zaidi kwasababu mashine nyingi zina uwezo mdogo, kwamfano ili mashine yako iweze kuingia windows xp inatakiwa iwe na angalau sifa hizi.

·  300 Mhz Intel or AMD CPU
·  128 Megabytes of system RAM (It can work with 64 Megabytes of RAM but its not recommended)
·  1.5 Gigabytes of available drive space
·  Super VGA 800x600 Display Adapter
·  CD or DVD-ROM
·  Keyboard and mouse, or other pointing devices
·  Network Interface Adapter required for Internet and Network Connectivity 
1.   Hakikisha una windows xp na funguo zake(keys) , na hizo key zinatakiwa zionekane kama hivi HHHCF-WCF9P-M3YCC-RXDXH-FC3C6. Kwasababu mbele utahitajika uziingize. 
2.  Lisome vizuri somo la kwanza kwasbb hatua hii inaeleza namna ya kuchagua boot order au boot sequence , mimi niliamua kufanya somo la pekee kwasbb ni kitu kirefu . Chagua boot sequence / boot order kama ulikuwa haujafanya hivyo. 
3Iingize Cd/Dvd yako , alafu bonyeza kifungo chochote kwasbb utakujia ujumbe huu “Press any key to boot from CD,"  , baada ya Cd kumaliza kusoma file zake, utatakiwa ubonyeze “Enter” ili uanze kuinstall windows os.

4.  Utatakiwa usome makubaliano ya matumizi(License Agreement) alafu ubonyeze F8 ili uoneshe kwamba umekubaliana na maelezo yao .
5.   Partition za harddisk zako zitaonekana, kwamfano C na D, unachotakiwa ni kuinstall windows katika disk c kwasababu ndio mara nyingi inatumika kama primary disk , hivyo itatakiwa uchague disk c, kama hard disk ndio unataka kuiweka os kwa mara ya kwanza hard disk yako itasomeka hivi "Unpartitioned Space." Utakachotakiwa ni kubonyeza kifungo chenye herufi  “C” ili uweze kutengeneza “partitioned”
6.   Ingiza saizi ya nafasi mpya ya partition yako(size in megabytes for the new partition) kama hautaki kuigawa ingiza namba hiyo hiyo itakayojitokeza, kama unataka vipande vingi na hii ndio njia bora yani operating system ikae kwenye disk yake na data zako zikae kwenye disk yake itatakiwa uingize saizi(megabyte ) unazozitaka kwaajili ya disk  ya kwanza na baadae utaingiza za disk ya pili, kumbuka disk unayotaka kuweka Os isipungue 1.5GB. baada ya kuingiza saizi uitakayo utabonyeza Enter.
7.  System itatengeneza  partition mpya, itafunguka tena windows  kwaajili ya kukuonesha partition zilizotengenezwa, utachotakiwa ni kuchagua partition ambayo unataka kuweka OS( windows xp) na mara nyingi inakuwa imeandikwa “C :“ baadae utabonyeza Enter. (kama harddisk yako inapartition hatua ya 6&7 iluke,  chagua tu disk unayotaka kuweka windows)
8. Chagua namna ya kuformat hard disk yako, ujumbe huu utakuja .                                        "Format the Partition using the NTFS File System(Quick)"                                                                           "Format the Partition using the FAT File System(Quick)"   
"Format the Partition using the NTFS File System"                                                                            "Format the Partition using the FAT File System"
Chagua    "Format the Partition using the NTFS File System" kwasababu inakubali nafasi kubwa na partition, tofauti na FAT, inakubali security features nyingi , pia inakubali compression  . kama unapatition zaidi ya 32 Gigabytes lazima utumie NTFS, lakini kama pertition ipo chini ya 32 Gigabytes unaweza kutumia FAT. Unaweza kuchagua FAT alafu baabae ukaibadilisha kwenda NTFS lakini hakuna uwezekano wa Kubadili NTFS kurudi FAT.

Haushauliwi kutumia quick format kwasababu italuka baadhi ya hatua muhimu kama kuangalia bad sectors n.k

Baada ya kuchagua utabonyeza Enter 
9.   System itaanza kuformat hardisk yako, lakini ni partion moja tu ambayo umeichagua kwaajili ya kuiingiza windows xp.
10.   Windows itaanza kukoppi faili(file) kukoka kwenye cd, na itataka kureboot/ restart  baadae, utatakiwa kubonyeza Enter au itajizima na kuwaka yenyewe baada ya sekunde 15.
11.   Wakati mashine inawaka italeta tena ujumbe huu “Press any key to boot from cd” tafadhali katika hatua hii usibonyeze kifungo chochote, narudia tena usibonyeze kifungo chochote iache mashine iboot kwa kutumia hard disk.
12.  Itafunguka window yenye rangi ya bluu na maelezo mengi upande wa kulia, wewe vuta subira tu(windows itaanza kwa kukuambia zimebakia dakika 39 mpaka kumaliza installation ).
13.  Baadae itatokea dialog window , itakutaka uchague nchi  uliyopo(Regional) na lugha.
14.   Baadae itatokea dialog window , itakutaka mashine uipatie jina( Andika jina lako).

15.   Itafunguka tena window nyingine na kukutaka uingize zile funguo zako (key)
16.   Baadae itatokea dialog window  nyingine, utaingiza password ya kuingilia kwenye windows yako(sio lazima).
17.   Utachagua ukanda wa muda(time zone),tarehe  na saa    
   
18.   Setup itaendelea kuinstall vifaa vilivyounganishwa kwenye mashine(peripherals devices) na jumbe mbali mbali zitapita upande wa kulia na baadae mashine itareboot kama mwanzo.
19.   Acha "Typical Settings"  katika setting za network ,labda kama umejifunza njia nyingine ya kuaccess network unaweza ukafanya mabadiliko.
20.  Hongera - Congratulations!  Umefanikiwa kuingiza windows Os

21.   Baada ya kureboot utaclick “yes” kukubaliana na visual settings to improve quality.

22.  Box linalofuata unaweza kulisoma na baadae utabonyeza “Ok” button

23.   (hatua hii na zinazofuata zinategemea aina ya windows hivyo si lazima ukutanenayo)Itatokea tena windows kama ya mwanzo na kukutaka ujiunganishe kwenye internet , utafanya hivyo.
24.   Baada ya kujiunganisha na internet utaActivate windows, chagua "Activate Now."
25.   Baada ya kuactivate itafunguka window ya kukutaka uingize-jina(username) yako, weka angalau moja.
26.   Tayari utakuwa unatumia default  default Windows XP Desktop. Congratulations!.. hangera  
                           


0 comments:

Post a Comment